Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke: Nimejitoa kuisaidia Simba

Baleke Hjks ???????Mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke.

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke amesema kwa hatua waliyofikia bado wana kazi kubwa iliyopo mbele yao na wanatakiwa kuendelea kupambana kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF).

Baleke alisajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo na tayari amesaidia timu hiyo katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kutikisa nyavu mara tano na tatu katika ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na gazeti hili jana, Baleke alisema anatambua wanaenda katika hatua ngumu ya robo fainali na kulazimika kupata matokeo mazuri ili kusonga mbele.

Alisema, michuano hiyo inawakutanisha na wachezaji wenye viwango tofauti na wanaocheza ligi tofauti hivyo watakuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwao.

“Binafsi nimejifunza vitu vikubwa zaidi na mengine ni siri yangu na yataonekana uwanjani wakati wa kusaidia timu yangu kwenye michuano iliyopo mbele yetu ikiwemo ligi ya ndani, kombe la Shirikisho na mechi mbili za hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Baleke.

Aliongeza: “Kufunga ni jukumu langu kila ninapopata nafasi ya kufanya hivyo, maana yangu ni kwamba tunacheza watu wengi uwanjani nikiona mchezaji mwenzangu yupo nafasi ya kufunga natoa pasi wote tunajenga Simba moja.”

Alisema hatakiwi kuwa mchoyo kwa mchezaji mwenzake anapokuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kusaidia timu kupata ushindi kwa sababu ana imani kubwa ya wachezaji walikuwepo Simba wanahitaji kufikia malengo yao.

“Mbele yetu tuna kazi nyingi tunapaswa kuelekeza nguvu kupambana kwa pamoja ya kutinga hatua ya nusu fainali ya CAF na tunapaswa kuongeza ushindani zaidi tufanikiwe, malengo yetu hayo,”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: