Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bajeti Simba, Yanga zawaibua wadau

Inonga Simba Yanga Bajeti Simba, Yanga zawaibua wadau

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya klabu za Simba na Yanga kutangaza bajeti zao kwa msimu ujao wa 2023/24, wadau wa soka nchini wamejitokeza na kueleza hisia zao huku wakikiri hatua kubwa zimepigwa japo bado kazi ipo.

Kwenye mdahalo wa 'Twitter Space' unaoendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), wadau walichangia kuhusu bajeti za klabu nchini zinakidhi mahitaji halisi kiushindani.

Akizungumzia hilo Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Issa Masoud alisema bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi ya timu husika hivyo kuna uwezekano yakafikia, yakapungua au yakazidi.

"Hii ni mfano unapokuwa na matumaini ya kufika nusu fainali na upate ile pesa ya CAF, zawadi ni kubwa ila matumizi pia huwa ni makubwa hivyo bajeti ni makadirio tu sio hiyo pesa tayari ipo."

Aidha Masoud aliongeza kwa udhamini na vyanzo ambavyo Simba na Yanga inazo anaamini inasaidia sana kupunguza changamoto za kiuendeshaji tofauti na ukilinganisha na timu nyingine za chini.

Kwa upande wa Mtaalamu wa Biashara, Masoko na Chapa, Biko Scanda alisema licha ya bajeti kubwa kwa timu hizo ila bado ni ndogo kwake na haziwezi kushindana na timu kutoka ukanda wa Kaskazini.

"Kuna wakati nilikuwa natembelea matumizi ya Al Ahly nikaona kwa mwezi wanatumia hadi zaidi ya Sh10 bilioni sasa utaona ni kwa jinsi gani wenzetu walivyotuacha mbali kwa kiasi kikubwa mno."

Aidha Scanda aliongeza endapo Simba na Yanga zitatengeneza wanachama zaidi ya milioni moja kwa mwaka kutokana na gharama ya Sh24, 000 wanazolipa itawasaidia kuongeza kipato tofauti na sasa.

Mjadala huu ulizuka baada ya Yanga kutangaza bajeti ya Sh20.8 bilioni huku Simba ikitangaza Sh23 bilioni ambazo watazitumia kwa msimu ujao wa 2023/2024 wa mashindano mbalimbali ya ndani na nje.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: