Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Simba wamtambulisha Kocha mpya wa Magolikipa

Daniel Cadena Simba.jpeg Daniel Cadena

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Jana Julai 5 Simba SC kutambulisha usajili wao wa kwanza kuelekea msimu ujao 2023/24 akiwa ni mshambuliaji Willy Essomba Onana.

Bado wekundu wa Msimbazi hawapoi kwani leo Julai 6 wamemtangaza Daniel Cadena kujiunga na Klabu hiyo kuwa Kocha wa Magolikipa akichukua nafasi ya Chlouha Zakaria alieachana na Simba mwezi uliopita.

Cadena amejiunga na Simba akitokea Azam FC alipodumu kwa mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2023.

Kwa Wasifu Cadena ana wasifu mkubwa akiwa amefundisha timu mbalimbali barani Ulaya, China pamoja na falme za Kiarabu kabla ya kuja Afrika.

Cadena amewahi kukionoa kikosi cha timu ya vijana ya Sevilla FC ya Hispania msimu wa 2018/2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: