Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BREAKING: Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba" Try Again" atangaza kujiuzulu

Capture545454 Aliekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah

Tue, 11 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salim Muhene "Try Again" ametangaza kujiuzulu wadhifa huo katika Klabu ya Simba leo Juni 11, 2024.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya wajumbe kadhaa kutangaza kuachia ngazi huku yeye ikisemekana kuwa amegoma kung'atuka madarakani.

Try Again amemuomba mwekezaji ndani ya Simba Mohammed Dewji kurejea na kuchukua wadhifa huo kwa ajili ya maendeleo ya Simba SC huku yeye akibaki kuwa Mwanachama wa kawaida.

Akizungumza Try again kupitia televisheni amesema;

“Kwa maslahi mapana ya Simba kwa kutambua mpira ni mchezo wa hisia, Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi nimemwomba Mwekezaji wetu Mohamed Dewji MO arejee kama Mwenyekiti wa Bodi nami nitasalia kama Mwanachama na Kiongozi ambaye nipo tayari wakati wowote kuitumikia Simba, kwa maana hiyo natangaza kuondoka kwenye kiti”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: