Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azama: Tumepitia mengi, ila leo....!

Kally Ongala Big Match Kally Ongala

Sun, 7 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Azam FC Kali Ongala amsema, timu yao ilipata fursa ya kucheza mechi mbili za kirafiki ili kuwaweka tayari wachezaji kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Simba.

Mchezo huo utapigwa leo Jumapili, Mei 7, 2023 katika Dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

"Tumecheza mechi mbili za kirafiki ambazo hazihusishi mashabiki [behind closed doors] kwa ajili ya kuwapa wachezaji utayari wa mechi.!"

"Tupo kwenye kipindi ambacho tunaelekea mwishoni mwa msimu, wachezaji wameshapitia mambo mengi kuanzia pre-season hadi hapa walipo, ndio maana hata wenzetu kikosi chao kilichocheza juzi kilikuwa na mabadiliko makubwa."

Mara ya mwisho Azam kucheza mechi ya ushindani ilikuwa ni Aprili 22, 2023 [Ruvu Shooting 1-3 Azam FC], Ongala amesema anawaamini wachezaji wake na timu yake kuelekea mchezo wa kesho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: