Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ambangile: Rafu ya Inonga, Haji Ugando hajafanya kosa la mauaji

Inonga Nje Wiki 2 Rafu ya Inonga, Haji Ugando hajafanya kosa la mauaji

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka Wasafi FM, George Ambangile amesema kuwa rafu aliyochezewa beki wa Simba SC, Henock Inonga kutoka kwa haji Ugando wa Coastal Union ni rafu ambazo zinachezwa mara kwa mara kwenye soka.

Ambangile amesema kuwa mashabiki wasiifanye kuonekana ndiyo rafu mbaya kuliko zote kwani hiyo si rafu ya mwisho kuchezwa kwenye soka hivyo tutegemee rafu kama hizo na mbaya zaidi ya hizo zitaendelea kuchezwa kwenye mpira wa miguu.

"Mimi siamini kama kuna mchezaji anaingia uwanjani kwa lengo tu la kwenda kumuumiza mchezaji mwenzake kwa makusudi.

"Tusimuongelee Haji Ugando Kama vile amefanya kosa la mauaji. Hii sio rafu ya Kwanza, naamini pia hii haitakuwa rafu ya mwisho zitatokea na zingine.

"Katika mpira Kuna Kipindi unakuta rafu hizo zinatokea tu katika kuwania mpira, mchezaji anaweza akachelewa katika kuwania mpira akatumia nguvu kubwa na ikapelekea kucheza rafu mbaya.

"Pia haimaanishi mchezaji akicheza rafu na yeye badae achezewe rafu. Huo utakuwa sio mpira sasa," amesema George Ambangile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: