Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Aliyeiua’ Prisons kwa Simba, aigeukia Yanga

Mlemavu Simba ‘Aliyeiua’ Prisons kwa Simba, aigeukia Yanga

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati presha ya mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga ikianza kupanda, shabiki lialia wa Wekundu, Aiwelo Simon ‘Kocha mlemavu wa dunia’ amesema liwake jua, inyeshe mvua lazima chama lake lishinde nyingi akiwashtua mabeki.

Shabiki huyo mkazi wa Tunduma mkoani Songwe alikuwa kivutio kwa benchi la ufundi la Simba chini ya Ko-cha mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ wakati wa mchezo wao na Tanzania Prisons waliposhinda 3-1.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Sokoine,Oktoba 5 ilishuhudiwa Robertinho na kocha wa makipa, Dan-iel Cardena wakipiga naye picha na kumuachia kiasi cha fedha ambacho hakikujulikana haraka.

Simba inatarajia kushuka uwanjani Novemba 5 kukiwasha dhidi ya watani zao, Yanga huku kila upande ukiwa na matumaini ya kushinda mchezo huo ili kujiweka pazuri kwenye msimamo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Simon alisema kutokana na umuhimu wa mchezo huo anatarajia kuwapo uwanja wa Taifa akisema kuwa tayari ameshaona timu yake ikishinda mabao yasiyopungua mawili.

Alisema yeye kama shabiki mkereketwa wa Wekundu ameangalia mchezo huo ameona ugumu wake akisema mabeki wanapaswa kuwa makini sana na wapinzani ambao wamekuwa na muendelezo mzuri wa kufunga mabao.

“Hata mechi dhidi ya Prisons nilisema mapema kuwa tutashinda kwa idadi ya mabao yasiyopungua mawili, nadhani kilichotokea kilionekana, hivyo basi Novemba 5 nitakuwapo Taifa na Simba itashinda,” alisema shabiki mwenye ulemavu.

Aliwaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani kuisapoti timu hiyo, akitamba kuwa msimu huu wanahitaji rekodi ya kumaliza ligi bila kupoteza na kutwaa taji ambalo wamelikosa kwa misimu miwili mfululizo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: