Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed: Simba tulieni., ubingwa upo palepale

Simba Wafunguka Madai Ya Phiri Kuondoka Simba Ahmed: Simba tulieni., ubingwa upo palepale

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kwamba timu hiyo bado ina nafasi kubwa ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC licha ya kufungwa bao 5-1 na wapinzani wao Yanga.

Ahmed amesema kuwa Simba imepoteza alama 3 tu sawa na Yanga, hivyo mashabiki wasikate tamaa kwani nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu ni kubwa na malengo yapo palepale.

"Simba ni timu kubwa, na ukubwa wetu utaonekana namna ambavyo tuta-react baada ya kufungwa. Kuna watu wanaeleza kana kwamba Simba kufungwa tumepiteza alama 30 wakati tumepoteza alama tatu tu ambazo hata mpinzani wetu amepoteza mchezo mmoja na wengine wamepoteza zaidi ya mchezo mmoja, kwa hiyo mzani ume-balance.

"Tumepoteza alama tatu bado kuna michezo 23 na alama 69 za kupigania. Simba malengo yetu ni kuangalia alama ambazo ziko mbele yetu, bado tuna nafasi ya kupambania ubingwa, jahazi la Simba halijatoboka, limepepesuka na sasa limekaa sawa, safari inaendelea.

"Simba ni timu kubwa, inapopoteza mchezo lazima izungumwez kwa ukuwa sababu ya ukubwa tulio nayo, tungekuwa na sifa ndogo kama Azam hakuna ambaye ngetuzungumzia, sisi tunaganga yajayo," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: