Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally awatuliza mashabiki wa Simba

Ahmed Ally Simbaz Vingu.jpeg Ahmed Ally awatuliza mashabiki wa Simba

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amewasihi mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa wanyonge kwa kulikosa Kombe la Mapinduzi, kwani wamefaidika zaidi na michuano hiyo kuliko vile walivyopoteza.

Ally amesema hayo alipowasili katika Bandari ya Jiji la Dar es Salaam, akitokea visiwani Zanzibar na kikosi cha Simba kushiriki Michuano ya 18 ya Mapinduzi.

"Kulikosa kombe la Mapinduzi, tumepoteza kitu kidogo mno kuliko faida tuliyoipata," amesema kiongozi huyo maarufu 'Semaji'.

Aidha, amezungumzia hali ya kikosi chao na kusema kama si leo basi kesho kuna wachezaji watakaoachwa kikosini na wale waliokamilishiwa uhamisho wao wa kuingia kikosini.

"Kabla ya tarehe 15, kila mmoja atafahamu hatma yake kabla dirisha halijafungwa." Amesema Meneja huyo.

Ahmed hakusita kuzungumzia kuimarika kwa kiwango cha kiungo wa klabu hiyo, Fabrice Ngoma ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano ya Mapinduzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: