Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally awaangukia mashabiki kisa matokeo mabovu

Simba Ahmed Mashabiki Ahmed Ally awaangukia mashabiki kisa matokeo mabovu

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewaomba mashabiki kuendelea kupa sapoti timu yao licha ya kupata matokeo mabaya kwenye mchezo wao wa jana.

Ahmed amesema hayo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC huku SImba SC wakikubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons katika Uwanja wa CCM Jamhuri Morogoro.

“Kuumia pasi na shaka wameumia, kila Mwanasimba ameumia kutokana na matokeo haya. Watu wa Morogoro watakuwa wameumia sana kwa sababu walikuwa na shauku ya kuiona Simba ya moto na walikuwa na matarajio na matumaini makubwa kwamba leo (jana) ile Simba ya hatari inakwenda kuiona mubadhara kwa macho yangu kwa matokeo haya wamekuwa disappointed.

“Lakini niwambie tu kwamba ndiyo matokeo ya mpira wa miguu, kuna wakati tunapata matokeo ya kutuumiza kama haya. Tuwaombe radhi wana Morogoro kwa hiki ambacho kimetokea. Tuendelea kuwaomba sapoti yao, mchango wao na nguvu yao kuendelea kuisapoti Simba yao.

“Tayari tumeshapoteza alama tatu, hata tukisema huyu hafai, huyu kafanya hivi, huyu vile, bado haiwezi kufuta matokeo ambayo tumeyapata.

“Tumeyapokea matokeo haya na kuangalia wapi kumekuwa na madhaifu kwa siku ya leo (jana) na kwenda kuyafanyia kazi katika michezo inayokuja. Ya leo yamewaumiza, lakini tugange yajayo, tusiiache timu peke yake pasi na mashabiki,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: