Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Yanga ina wachezaji bora kuliko Azam, wa kwetu ni bora kuliko Yanga

Ahmed Ally 5 Nov Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Mechi ya Simba na Yanga huwa ni mechi ngumu huwa haijalishi timu zote zipo kwenye hali gani. Hata mashabiki wa Simba tukicheza dhidi ya mashabiki wa Yanga unaona kabisa amsha amsha jinsi ilivyo."

"Hata kama Yanga awe vibaya kiasi gani wanaweza wakasafiri na lori kwenda mpaka Mbeya sababu ya kupitia hali ngumu lakini bado wakicheza dhidi yetu mechi huwa ni ngumu."

"Licha ya kufungwa na Ihefu ambayo imeshazoea kuwafunga Yanga, bado mechi yetu dhidi yao huwa ni mechi ngumu. Na ukiangalia mfululizo wa mechi zao kwasasa unaona kabisa itakuwa mechi ngumu."

"Lakini tutawafunga sababu sisi Simba tuna wachezaji wenye ubora kuliko wachezaji wao. Yanga wana wachezaji wenye ubora lakini ukiwalinganisha na wachezaji wa Simba, sisi ndiyo tuna wachezaji wenye ubora zaidi kuliko wote."

"Yanga wana wachezaji wenye ubora kuliko wa Azam, wa Azam wana ubora kuliko Mashujaa na sisi tuna wachezaji wenye ubora zaidi kuliko hao wote, tuna wachezaji wenye ubora wa ngazi ya Afrika. Kama wachezaji wa Simba wakiamua mechi hii tunataka kushinda basi hakuna timu inaweza kutuzuia."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: