Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Wydad akija kwa Mkapa ni kumkamua tu

Ahmed Ally Press Leo.jpeg Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC imesema wazi kabisa ili kuhakikisha wanatoboa kwa hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Afrika hawana budi kuhakikisha wanakufa na Wydad Casablanca katika michezo yao miwili inayofuata.

Simba wameanza hatua ya makundi kwa sare mbili mfululizo na hivyo wanahitaji ushindi kufufua matumaini ya kusonga mbele.

Akizungumza kupitia kipindi cha Sports Extra, Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally anasema;

“Ukiangalia msimamo wa kundi hautupi presha ya kutunyima pumzi kwamba lazima tupate alama tatu ,tukipata alama moja mbele ya Wydad tunakuwa tumejiweka kwenye nafasi nzuri mno”

“Tumebakisha mechi mbili hapa nyumbani ,Wydad akija hapa nyumbani hakuna option mbili option ni moja tu kumkamua ,akija tena Jwaneng tunamkamua atuachie alama tatu ,hapo tutakuwa tumefikisha alama 6 na tatu za ugenini tutakuwa na 9 mnyama anaenda Robo fainali”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: