Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Waarabu tutamalizana nao huko huko!

Simba Kikosi Kwenda Misri Ahmed Ally.

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, amesema hawatawafuata wapinzani wao Al Ahly kinyonge bali wanakwenda kifua mbele wakiamini watafanya maajabu ugenini.

Kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya pili ya Africa Football League, Simba inahitaji ushindi kusonga mbele baada ya kushuhudia ubao ukisoma Simba 2-2 Al Ahly, robo fainali ya kwanza iliyochezwa juzi Ijumaa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza nasi, Ally alisema wakubwa hawana hofu ya kucheza mechi kubwa ugenini ama nyumbani, wanachotafuta ni ushindi.

“Hakuna asiyetambua ukubwa wa Simba ndio maana tupo kwenye timu 8 kubwa Afrika, kushindwa kupata ushindi hapa tunakwenda kuwafuata hukohuko kumalizana nao Misri.

“Sio kinyonge tena bali kazi yetu kubwa ni kutafuta ushindi kwenye mchezo wa robo fainali ya ugenini. Haitakuwa kazi nyepesi, lakini hatuna hofu tunajiamini na tunakwenda kufanya kweli.

“Mashabiki ni muda wa kuendelea kutamba kutokana na hatua ambayo tupo, wachezaji wanajituma nadhani mliwaona akina Kibu Denis, Jean Baleke, Saidi Ntibazonkiza akina Clatous Chama walivyokuwa wakitoa burudani,” alisema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: