Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Mechi tunaimaliza Dar, uwezo wa kushikilia Bomba tunao

Ahmed Ally LEO Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchikha ni miongoni mwa silaha zetu muhimu kuelekea mchezo wetu wa Machi 29, 2024 (Simba V/s Al Ahly), Benchikha ni kocha mkubwa mwenye wasifu mkubwa ambaye anaweza kucheza mechi kama hizi.

Ndio maana nasema, kwetu mechi hii ni ya mkondo mmoja tu! Tutahangaika kuhakikisha tunaimaliza hii mechi Dar es Salaam.

Uwezo wa kushikilia bomba ‘kuzuia/kujilinda’ Simba tunao, tuliona hapa dhidi ya Wydad tulishinda 2-0 tukashikilia bomba mpaka mechi ikaisha.

Kule nyumbani kwao [Wydad] tulishikilia bomba mpaka dakika ya 93, makosa madogo yakapelekea tukaadhibiwa. Simba hatuwezi kuzuiliwa na Al Ahly, wanasimba tumeamua jambo letu, Al Ahly anafia Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: