Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Kuna watu wataishi maisha ya shida wiki hii

Ahmed Ally Simbaz Vingu.jpeg Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo matano aliyoyaongea Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu ya Simba Sc, Ahmed Ally katika hamasa waliyoifanya Viwanja vya Manzese kuelekea mchezo wa African Football League dhidi ya Al Ahly ya Misri

"Ni heshima kubwa Simba tumepewa kuandaa mechi ya ufunguzi wa mashindano haya kwa mara ya kwanza."

"Wengine wataishi maisha ya shida sana wiki hii, na sisi sio shida zetu tutazidisha dozi."

"Tumepewa wenyeji wa michuano hii sababu ya ubora ambao tupo nao, zipo timu nyingi Tanzania, zipo timu nyingi Afrika lakini walikaa kujadili timu gani inafaa wakaona Simba Sports Club."

"Hatujapata nafasi hii kwa bahati mbaya, tumepata kwa ubora tulionao. Kama sio Simba kuwepo Tanzania basi Tanzania kusingekuwa na timu inayoshiriki African Football League kwa sababu baada ya Simba hakuna mwingine mwenye mafanikio kimataifa zaidi yetu."

"Ukweli unabaki kuwa sisi Wenye Nchi ndio tumeleta AFL hapa. Wanasimba mna nafasi kubwa ya kujipongeza, kufurahi sababu tumekomboa nchi kupata nafasi ya michuano hii, na kwenda mbali zaidi ya kuwa mwenyeji wa michuano." amesema Ahmed

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: