Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Huyu Fabrice Ngoma ni habari nyingine

Fabrice Ngoma Na Ahmed Ally Ahmed Ally: Huyu Fabrice Ngoma ni habari nyingine

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba SC umebainisha kuwa kiungo mpya Fabrice Ngoma ana balaa akiwa uwanjani kwa kufanya kazi tatu kwa wakati mmoja akitimiza majukumu yake.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema, kuwa kiungo huyo atawapa burudani Wanasimba kwenye mechi zote atakazocheza.

“Hapa ninataka kumgusia kidogo tu Fabrice Ngoma huyu ana balaa akiwa uwanjani, anacheza kisha anatoa maelekezo wa wenzake, halafu ana uzoefu mkubwa wa mechi za kitaifa na kimataifa umeona tulivyopata mchezaji mzuri.

“Kuwa na Ngoma ni mwanzo tu, anapocheza anampa maelekezo Mzamiru Yassin kisha nenda pale pasi inakuja na akisema hivyo ni uhakika pasi inafika na anatuliza timu burudani zinakuja Wanasimba watafurahi.

“Ameicheza AS Vita ile yenyewe yamoto kabisa ambayo Simba SC tuliifunga, amecheza Raja Casablanca hivyo ana uwezo mkubwa na hadhi ya kuwa ndani ya Simba SC hcbu fikiria katikati una Sadio Kanoute una Mzamiru Yassin, una Onana “unadhani nini kitatokea?” amesema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: