Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Benchikha yupo sana Simba SC

Benchikha WA0006 Ahmed Ally: Benchikha yupo sana Simba SC

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Klabu ya Simba SC umesema hauna mpango wowote wa kuachana na kocha wao, Abdelhak Benchikha, kama inavyoanza kuvumishwa na baadhi ya watu, huku ikiweka wazi kuwa tayari imeshakutana naye kwa ajili ya kujadili tathimini ya maboresho ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu

Kauli hiyo inakuja baada ya kuwapo kwa taarifa katika Mitandao ya Kijamii na baadhi ya wachambuzi wa soka juu ya kocha huyo, wakidai yupo hatarini kutupiwa virago kuondoka ndani ya timu hiyo baada ya matokeo mabovu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema hakuna ukweli juu ya nia yoyote au mpango wa kumtimua au kusitisha mkataba na Benchikha kwani ni kocha mkubwa Afrika na wanamuamini.

Amewataka mashabiki kutulia kwa kipindi hiki cha mpito na kuimarisha nguvu na mshikamano kwa ajili ya kuimarisha timu yao kwa msimu ujao kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Benchikha.

TPLB: Ratiba Ligi Kuu haitavurugwa

“Hatuna mpango huo wa kumuondoa au kuachana na Benchikha, Wanasimba wanatakiwa kupuuza taarifa zilizosambaa kuhusu kocha wetu, kwani lengoletu ni kuhakikisha kocha huyu anakuwepo klabuni hapa ili tuhakjikishe tunakuwa na kiokosi bora ambacho kitakuwa tishio katika Michuano ya ndani na ile ya Kimataifa.”

“Benchikha yupo sana na jana Jumanne (Aprili 23) mchana alikuwa sehemu ya timu iliyoenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Muungano ikiwa ni sehemu ya mipango ya kuhakikisha tunafanikiwa kushinda kombe hilo,” amesema Ahmed

Ameongeza kuwa kikosi kipo vizuri na wachezaji wote wako salama na wako kwenye msafara huo kasoro wawili, beki Shamari Kapombe, aliyeumia kwenye mazoezi ya kujianda na michezo ya Kombe la Muungano.

Ahmed amesema mchezaji mwingine ambaye hajaambatana na timu ni kiungo Sadio Kanoute mwenye majeraha baada ya kuumia kwenye mchezo wa dhidi ya Young Africans mwishoni mwa juma lililopita.

Amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya michuano hiyo ya Kombe la Muungano kwa kufanya vizuri katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali dhidi ya KVZ FC ya visiwani humo.

Simba SC leo Jumatano (Aprili 24) saa 2:15 usiku itamenyana na wenyeji, KVZ katika Nusu fainali ya Kombe la Muungano, itakayopigwa Uwanja wa New Amaan Complex visiwani, Zanzibar wakati Azam FC kesho Alhamisi (Aprili 25) itavaava na KMKM, na Washindi wa mechi za hizo za watakutana katika Fainali ya michuano hiyo Aprili 27, mwaka huu uwanjani hapo.

Chanzo: Dar24
Related Articles: