Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahly waitangulia Simba kwa Mkapa

Simba Kikao Na Mo Dewji.jpeg Ahly waitangulia Simba kwa Mkapa

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wageni Al Ahly ndio timu ya kwanza kutinga Uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa na msafara mkubwa kuliko wenyeji.

Ahly wameingia Uwanja wa Mkapa saa 10:01 jioni wakiwa kwenye basi lao kubwa moja huku pia wakiwa na mabasi madogo mawili na gari ndogo tano.

Baada ya Ahly kufika dakika tano baadaye wenyeji wa mchezo Simba wakafuata nyuma wakifika taratibu huku mashabiki wao waliopo nje ya uwanja wakiwashangilia kwa nguvu

Simba walitinga uwanjani wakiwa na msafara wa magari yao manne tu likiwemo basi lao kubwa lililofanyiwa urembo vizuri na gari ndogo tatu.

Kila timu ilipita njia yake wakati wa kuingia uwanjani ambapo hakukuwa na vurugu zozote huku ulinzi ukiwa mkubwa kwa kila timu kuingia wakiwa kwenye pikipiki maalum ya Polisi ikihashiria kila kitu cha usalama kipo sawasawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: