Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Bao la Makelele liliiokoa Simba 1988

Makeleleeee Bao la Makelele liliiokoa Simba 1988

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hii stori haizungumzwi sana. Lakini klabu ya Simba ya Dar es Salaam iliwahi kuponea chupuchupu kushuka daraja kwa misimu miwili mfululizo.

Wakati huo Ligi Kuu ya Tanzania ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza, Simba ilinusurika kushuka daraja na ingetakiwa kucheza Ligi daraja la Pili (sasa Championship) msimu uliofuata.

Bahati mbaya hii iliikuta Simba zaidi ya mara moja! Kwani iliponea katika tundu la sindano mara mbili. Bundi wa kutaka kuishusha timu hiyo daraja alianza kuiandama mwaka 1988 na baadaye mwaka 1989.

Mwaka 1988, Simba ilikuwa katika hali mbaya hadi dakika za mwisho kabisa wakati ligi ikielekea ukingoni.

Katika ratiba zilikuwa zimebaki mechi mbili ngumu moja ikiwa ni dhidi ya Pamba ya Mwanza jijini Mwanza na nyingine dhidi ya Yanga SC jijini Dar es Salaam.

VIGOGO WAGAWANA MECHI

Simba ilifikia hatua hiyo kutokana na mgogoro mkubwa uliokuwa ikiitafuna ndani kwa ndani na kuwafanya viongozi kugawanyika katika pande mbili. Ilifikia hatua viongozi walioigawa timu hiyo vipande viwili waliitwa na wazee na kushauriwa kugawana mechi mbili zilizobaki.

Kila mmoja alitakiwa kuchagua mechi moja ali aweze kuinusuru timu isishuke daraja.

Viongozi hao walikuwa ni Katibu Mkuu wa Simba, Jimmy David Ngonya na aliyekuwa mfadhili wa timu hiyo, Jabiri Sikamkono (siyo Shikamkono kama ilivyozoeleka). Ngonya alikuwa wa kwanza na alichagua mechi dhidi ya Pamba iliyokuwa inafanyika CCM Kirumba na Sikamkono hakuwa na budi kukubali kusimamia mechi dhidi ya Yanga ya jijini Dar es Salaam.

YAPIGWA NA PAMBA

Ngonya alikuwa na mategemeo makubwa ya kushinda mchezo dhidi ya Pamba na kuibakisha timu katika ligi.

Siyo peke yake, kila mtu alikuwa akiiona salama ya Simba ni kushinda dhidi ya Pamba na kuibakisha kwenye ligi huku wakitarajia matokeo yoyote katika mchezo uliokuwa unafuata dhidi ya mtani wake, Yanga.

Lakini matumaini ya kubaki Ligi Daraja la Kwanza yalitoweka baada ya Simba kupoteza mchezo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza dhidi ya Pamba.

MAKELELE AOKOA JAHAZI

Katika mchezo mchezo uliopigwa Julai 23, 1988 katika Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) jijini Dar es Salaam dhidi ya Yanga ndipo Simba iliponusurika. Simba ilitakiwa kushinda mchezo huo ili kunusurika kushuka daraja na Yanga ilitaka ushindi ili ibebe ubingwa wa ligi.

Marehemu John Makelele aliokoa Simba kushuka daraja baada ya kuifungia Simba bao la ushindi dhidi ya Yanga.

Baada ya ushindi huo, Yanga ilikosa ubingwa wa ligi na Coastal Union ya Tanga akawa bingwa rasmi wa Tanzania Bara.

Ulikuwa msimu wa Tanga kwani mwaka huohuo African Sports'Wana Kimanumanu', wapinzani wakubwa wa Coastal Unuion 'Wagosi wa Kaya' wakaenda kuandika historia kwa kutwaa ubingwa wa Muungano.

LAWAMA ZOTE KWA SAHAU

Katika mchezo dhidi ya Yanga, Simba ilitangulia kufunga bao lililowekwa kimiani na Edward Chumila 'Smailling Killer' katika dakika ya 21 na Yanga ikachomoa kupitia kwa Issa Athumani Mgaya ‘Seketawa’ katika dakika ya 36.

Hata kama mchezo ungeisha kwa matokeo hayo, bado Simba ingeshuka daraja lakini katika dakika ya 58, John Makelele ‘Zigzag’ alifunga bao la ukombozi na kuifanya Simba kupata uhai wa kubaki Ligi Daraja la Kwanza.

Bao hilo la ushindi lilimpa tabu sana kipa wa Yanga, Sahau Kambi ( Kipa wa kwanza kuitwa Tanzania One) kutoakana na kutema shuli lilipigwa langoni mwake na kumfanya Makelele kumalizia kwa urahisi.

Mojawapo ya gazeti maarufu wakati huo, lilichochea habari hiyo kwa kutoa picha ya Sahau Kambi akiwa amelala chini wakati mpira ukiwa kimiani.

MINZIRO ATAKA KUZICHAPA

Mbaya zaidi picha hiyo ilisindikizwa na kichwa cha habari kilichosomeka ‘Ambavyo Sahau hatasau’.

Beki wa pembeni wa Yanga wakati huo, Freddy Felix ‘Minziro’ Baba Isaya au Majeshi alimfuata Sahau Kambi mara baada ya Makalele kufunga bao hilo na kutaka kuzichapa naye kwa kuhisi kwamba alikuwa ameiachia Simba bao hilo.

Mwaka 1989, Simba ilinusurika tena kushuka daraja, tena baada ya timu kadhaa kupanga matokeo ambayo yalikuja kufutwa baadaye.

Columnist: Mwanaspoti
Related Articles: