Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia awalilia waliokufa kwa mafuriko Hanang, atoa maelekezo

Samiaa Ikulu E Rais Samia awalilia waliokufa kwa mafuriko Hanang, atoa maelekezo

Sun, 3 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole na kutoa maelekezo kwa vyombo vinavyoshughulikia maafa yaliyotokea katika kijiji cha Katesh, Wilayani Hanang mkoani Manyara.

''Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kutokea kwa mvua kubwa katika mkoa wa Manyara na kuleta madhara makubwa katika kijiji cha Katesh,mimi na wenzangu tunatoa pole sana.''

Amesema ametoa maelekezo nguvu zote za serikali zielekezwe huko kwenye shughuli za uokoaji ili kuzuia maafa zaidi kutokea.

''Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tayari nimevielekeza vifike huko, wizara ya afya kushughulikia majeruhi,lakini pia wizara ya madini kuona kinachorokea katika sehemu ambayo milima imeonesha kutetemeka, imeonesha kuporomoka'' alisema Rais Samia.

Mpaka sasa watu 23 wamepoteza maisha na miili yao imepatikana huku wengine 30 kujeruhiwa kutokana na mafuriko katika eneo la Katesh na Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara, Gazeti la Mwananchi limeripoti.

Taarifa za awali zinasema kuporomoka kwa sehemu ya Mlima Hanang ndio chanzo cha mafuriko hayo. Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo jumapili imesababisha mafuriko ya tope katika eneo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: