Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokufa maafa ya Hanang wafikia 76

Wapangajiiii Hanang (600 X 272) Waliokufa maafa ya Hanang wafikia 76

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia jana mchana Desemba 07,2023 Watu 76 wamefariki Wilayani Hanang Mkoani Manyara kutokana na maafa ya mafuriko yaliyotokea.

Akiongea na Wananchinwa Hanang, Rais Samia amenukuliwa akisema “Janga hili limegharimu maisha ya Watanzania wenzetu 76 mpaka taarifa niliyoipata mchana lakini pia limeharibu makazi ya Wananchi wengi tu lakini pia tumekuwa na majeruhi nimetoka kuwatembelea Hospitali na tunashukuru Mungu wanaendelea vizuri”

“Kwa ujumla janga hili limeharibu miundombinu ya barabara, umeme, maji na mambo mengine, kwahiyo ni janga kubwa ambalo limelikumba Taifa letu.

“Nawashukuru Watanzania waliotoa msaada kwa njia moja au nyingine, huu ndio upendo tunaozungumza siku zote, janga lilipotokea nilikuwa safarini.

"Taarifa zimetoka wenzetu kule wamesikia na kwahiyo wenzetu kule wengi tu Mashirika yaliyokuwepo kule wametuchangia kiasi cha Tsh. bilioni 2.5 na nimeelekeza waziingize benki,” alisema Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: