Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Tennis

Yanga yakubali ombi la SportPesa

Ligi Kuu Nbc League Yanga yakubali ombi la SportPesa

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeridhia ombi mdhamini wao Sportpesa kuhitaji makombe waliyopata msimu wa 2023/2024 kupelekwa kwenye ofisi hizo ikiwa sehemu ya kutambua mchango wao katika miaka saba ya udhamini wao.

Kauli hiyo imetolewa leo baada ya Yanga kukabidhiwa na Sportpesa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh million 537.5 ikiwa ni sehemu ya bonasi ya mafanikio ya msimu wa 2023/24 ulitamatika hivi karibuni.

Hundi hiyo wamekabidhiwa leo na wadhamini wao Sportpesa baada ya kufanikisha malengo yao ikiwemo kutetea mataji ya mawili kwa msimu huu ikiwemo Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la CRDB.

Akizungumza nasi, Rais wa Yanga, Hersi Said amesema wamepokea na kufanyia kazi maombi ya wadhamini hao kuhakikisha wanapeleka makombe hayo siku ya Jumatatu katika ofisi ya wadhamini hao.

Amesema wanajivunia kushirikiana na Sportpesa, wanaendelea kutengeneza mahusiano mazuri na kampuni hiyo na kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwa namba moja Tanzania.

“Nichukue nafasi hii kuishukuru SportsPesa kwa kutekeleza kwa wakati makubaliano yaliyopo kwenye mkataba kwa kutoa bonasi baada ya klabu yetu kutwaa ubingwa huu Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho, tumefurahi sana kupokea rasmi zawadi hii ya bonasi,” amesema Hersi.

Ameongeza kuwa wanaahidi wataendelea kuijenga timu imara na ushindani mkubwa ndani na nje ya Tanzania ikiwemo kufikia malengo ya kutaka kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu ujao.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo Tarimba Abass, amesema bonasi hiyo ni baada ya klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho na Robo Fainali CAFCL msimu wa 2023/24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: