Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marefa hawa kuamua mechi za Yanga, Simba kimataifa

Marefaaaaa Marefa hawa kuamua mechi za Yanga, Simba kimataifa

Wed, 18 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Marefa kutoka Guinea na Mauritania ndio wamepangwa kuchezesha mechi za nyumbani za wawakilishi wa Tanzania Simba na Yanga katika mechi zao za marudiano za raundi ya pili ya mashindano ya klabu Afrika.

Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba dhidi ya Al Ahly Tripoli utachezeshwa na refa Abdoulaye Manet kutoka Guinea mwenye umri wa miaka 34.

Manet atasaidiwa na Waguinea wenzake ambao ni Sidiki Sidibe, Yamoussa Sylla na Bangaly Konate.

Huo ni mchezo wa kwanza wa mashindano ya klabu Afrika kwa Manet kuchezesha ambapo kabla ya hapo kitu pekee cha kujivunia kwa refa huyo kilikuwa ni kuwa refa wa akiba.

Katika mchezo huo, Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya timu hizo kutoka sare tasa katika mchezo wakwanza uliofanyika Libya, Jumapili iliyopita.

Mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00, Jumapili.

Refa wa kati kutoka Mauritania, Abdel Aziz Bouh yeye ameteuliwa na Caf kuchezesha mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na CBE ya Ethiopia.

Mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar siku ya Jumamosi, Septemba 22 kuanzia saa 2:30 usiku.

Bouh (32) atasaidiwa na raia wenzake wa Mauritania, Brahim H’Made, Mohamed Youssef na Diou Moussa kuchezesha mechi hiyo ambayo Yanga inahitaji angalau matokeo ya sare tu ili iweze kusonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 ugenini Jumamosi iliyopita.

Yanga inamkumbuka vyema refa Bouh kwani ndiye alichezesha mechi yao ya nyumbani ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly.

Katika mechi nane zilizopita za mashindano ga klabu Afrika, Bouh ametoa idadi ya kadi 24 ikiwa ni wastani wa kadi tatu kwa mchezo na katika hizo, kadi moja tu ndio nyekundu.

Msimu uliopita, Yanga na Simba zote zilifanikiwa kuingia hatua ya makundi na zilitolewa katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu Afrika ambapo zote zilikuwa zinacheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ilitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wakati Simba ilitolewa na Al Ahly ya Misri.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: