Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera atua kwa Lomalisa Mutambala

Lomalisa X Zahera Zahera atua kwa Lomalisa Mutambala

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuitumikia Yanga kwa misimu miwili, beki Mkongomani, Joyce Lomalisa anatajwa kutua Namungo FC kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Lomalisa awali alikuwa anatajwa kujiunga Simba lakini mambo yakaenda tofauti na sasa inaelezwa Namungo inayonolewa na Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera ina mpango wa kumpa mkataba wa miaka miwili staa huyo mwenye mataji mawili ya Ligi Kuu Bara.

Beki huyo mwenye uwezo wa kuanzisha mashambulizi na kupiga krosi zinazofika katika maeneo sahihi, pia ameshinda mataji mawili ya Kombe la Shirikisho (FA) akiwa na Yanga na kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023.

Zahera anataka kuijenga Namungo kuwa tishio msimu ujao na anasaka wachezaji wenye uzoefu na mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara watakaoifanya timu hiyo kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: