Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yule kipa wa Azam wanakwenda naye kimataifa? - Mchambuzi

Dg Zuberi Foba Yule kipa wa Azam wanakwenda naye kimataifa? - Mchambuzi

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtangazaji wa masuala ya michezo nchini, Alex Luambano amedai kuwa kiwango cha kipa wa Azam FC aliyedaka mechi dhidi ya Yanga jana ni hafifu na kwamba hana ubora wa kucheza kwenye mechi za kimataifa.

Luambano amesema hayo baada ya kipa huyo kuonyesha madhaifu mengi uwanjani kwenye mchezo wao wa Nusu fainali ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga Sc na kupoteza kwa bao 2-0 dakika za majeruhi.

Zuberi Foba (21) bado ni kipa mdogo hana uzoefu wa kutosha kucheza mechi kubwa zenye presha, licha ya kuwa na kipaji kizuri, hivyo anahitaji kujifunza zaidi kabla ya kuanza kuaminiwa na walimu.

Yanga imetumia dakika 5 tu kuamua mchezo huo kwa mabao ya kiungo mshambuliaji, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89.

"Kipa yule kazi anayo, ndio huyo wanaenda naye kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika yule?," amesema Luambano.

Yanga sasa inasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Singoida Fountain Gate na Simba, ambaye atashinda watakutana kwenye fainali huku Azam akisubiri atakayeshindwa mchezo wa leo atakutana naye kwenye mchezo wa mshindi wa tatu.

MECHI 6 ZA MWISHO Yanga v. Azam

• Yanga SC 2:0 Azam FC • Yanga SC 1:0 Azam FC • Azam FC 2:3 Yanga SC • Yanga SC 2:2 Azam FC • Azam FC 1:2 Yanga SC • Yanga SC 2:0 Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: