Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Young Africans yaanika ishu ya Mayele

Mayele Pyramids 27 Instagram Fiston Mayele

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umesema kuondoka kwa Fiston Mayele ni hatua ya kukua kwa soka ndani ya timu yao na watampata mbadala wake kwa kuwa maisha ni lazima yaendelee.

Mayele mchezaji na mfungaji bora msimu uliopita 2022/23 ametambulishwa rasmi na klabu ya Pyramids ya nchini Misri na kufunga mjadala wa tetesi za kuondoka kwake Jangwani.

Mkurugenzi wa Mashindano Young Africans, Saad Kawemba, amesema kuwa, katika klabu ya mpira mambo ya kuuza wachezaji ni kawaida pale ikitokea ofa yenye manufaa zaidi kwa mchezaji hawawezi kumkatalia kuondoka.

“Maisha ndivyo yalivyo leo hapa kesho pale, wanayanga walimpenda na alitufanyia makubwa kwa kushirikiana na wenzake lakini kujaribu maisha kwingine sio shida,”

“Mayele ataendelea kuwa Mayele tutampata mwingine mzuri ambaye hata kama hatofanana na Mayele lakini atakuwa bora,”amesema Kawemba.

Amesema Young Africans imesajili na ina wachezaji wote bora ambao watawavusha katika malengo yao ambayo wamejiwekea.

Katika hatua nyingine Kawemba amesema, msimu ujao wanajua ushindani utakuwa mkubwa ila wanajipanga kuhakikisha wanayatetea kwa mara nyingine makombe yote waliyoyatwa msimu uliopita.

Young Africans ilifanya vizuri msimu uliopita 2022/23 kwa kutwaa taji la mchezo wa hisani, Ligi Kuu, Kombe Shirikisho la Tanzania Bara ‘SAFC’ huku ikifika fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Chanzo: Dar24
Related Articles: