Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yasmine: Mchezaji hatakiwi kuwa na meneja, wa nini?

Fei Totooo.jpeg Fei Toto

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimamizi wa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' katika kesi yake na waajiri wake, Jasmine Razack amesema kuwa mchezaji anapaswa kuwa na Wakala na si Meneja kama wengi wanavyofanya.

“Sasa hivi kila ukimuuliza mchezaji unawasimamizi anakwambia nina meneja, kwani mchezaji ni msanii? Meneja wa nini? Mchezaji anapaswa kuwa na wakala [agent].”

“Hawa wasimamizi wa wachezaji wanapaswa kuhakikisha wana mwanasheria aliyebobea kwenye sheria za michezo kwa sababu sio kila mwanasheria amebobea kwenye sheria za michezo [Sports Law].”

“Japo English ndio lugha ya FIFA lakini mchezaji anaweza kuomba mkataba kwa lugha ya Kiswahili kama haelewi English.”

“Na mchezaji anaweza kuweka kipengele kuwa endapo ikitokea kutoelewana kati ya mchezaji na klabu, mkataba wa Kiswahili ndio utasimama kwenye chombo chochote cha usuluhishi,” amesema Jasmine Razack, Msimamizi wa Feisal Salum.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: