Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaweka wazi dau la Fei Toto, wamepiga au wamepigwa?

Feisal Azam  KL.jpeg Fei Toto akitambulishwa Azam FC akitokea Yanga

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imetangazo mapata ya mauzo ya wachezaji waliyowapata msimu uliyopita huku mchezaji aliyeuzwa ni kiungo Feisal Salum

Yanga ilimuuza Feitoto kwa Azam FC kwa dau lililofichwa kwa pande hizo mbili, lakini waliwekeana vipengele ambavyo timu hizo zitaendelea kunufaishana kwa mchezaji huyo.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Fedha, Sabri Sadick amesema bajeti ya mapato na matumizi iliyotumika msimu uliopita huku akitaja mapato waliyoyapata kwa upande wa mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kwa mchezaji Feisal Salum 'Fei Toto' kwenda Azam ambapo awali dili lake halikuwekwa wazi.

"Mauzo ya wachezaji ni Sh200 milioni kama mnavyojua tumeweza kumuuza Feisal Salum 'feitoto" amesema Sabri

Feisal amesaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamfanya akae kwenye timu hiyo ya Chamazi hadi 2026.

Kwa Mantiki hiyo Fei Toto ameiingizia Yanga Milioni 200 je wamepiga au wamepigwa? Tuachie maoni Yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: