Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yawasili salama Malawi

IMG 20230705 WA0171 Yanga yawasili salama Malawi

Wed, 5 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa mara 29 wa soka Tanzania Bara na mabingwa watetezi wa NBCPL, Klabu ya Yanga wamewasili nchini Malawi ambapo tumealikwa kwenye maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa nchi yao.



Kikosi hicho kilichoondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kwa ndege maalum kimewasili jijini Lilongwe tayari kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Nyasa Big Bullets utakaopigwa kwenye dimba la Bingu Mutharika kesho majira ya saa 10.



Yanga wamewasili nchim=ni humo wakiongozwa na Rais wa Klabu hiyo, Eng. Hersi Said. Kikosi kilichoondoka kimejumuisha wachezaji wa timu kubwa na wale wa Yanga B.



Mgeni maalum kwenye sherehe hizi kutoka Tanzania ni pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: