Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatumia njia za kimafia kusajili

Yanga Adhabu CAF Yanga yatumia njia za kimafia kusajili

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga imekuja na staili mpya ya usajili na sasa kama mchezaji haujafanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo, kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya basi fahamu imekula kwako, kwani hautakuwa sehemu ya wachezaji wa katika msimu ujao.

Wachezaji wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu ni, Bernard Morrison, Ibrahim Bacca, Metacha Mnata, Jesus Moloko, Crispin Ngushi, Denis Nkane, Eric Johora, Dickson Ambundo na Tuisila Kisinda anayemaliza mkataba wake wa mkopo wa mwaka mmoja.

Timu hiyo, tayari imewaongezea wachezaji wake watatu mikataba mipya ya kuendelea kukipiga hapo Khalid Aucho, Djigui Diara na Dickson Job ambao walisaini hivi karibuni.

Taarifa ambazo tumezipata, mabosi wa Yanga tayari wana orodha ya wachezaji ambao Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mtunisia Nasreddine Nabi amependekeza waendelee kuwepo hapo baada ya kuvutiwa na ubora wao.

Bosi huyo alisema kuwa wachezaji wote waliopendekezwa waendelee kubakia hapo, kati ya hao ambao hawajapewa mikataba mipya baadhi ni Bacca, Metacha na Moloko waliokuwepo katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kimyakimya kukamilisha dili hilo.

Aliongeza kuwa kama kuna mchezaji ambaye hajafanya mazungumzo yoyote na kuongeza mkataba na uongozi, basi hatakuwa sehemu ya wachezaji watakaobakia kuichezea timu hiyo.

“Usajili wa sasa ndani ya Yanga ni wa kimyakimya, anaitwa mchezaji na viongozi na kufanya mazungumzo kwa ajili ya kuongezewa mkataba mpya na kama haujaitwa au haujapewa mkataba mpya, basi mchezaji huyo hatakuwa sehemu ya wachezaji wetu msimu ujao.

“Wapo baadhi ya wachezaji ambao wao tayari tumewasajili kwa kuwapa mikataba mipya na kati ya hao ni Diarra, Job na Aucho, hivi sasa tunamalizana na wengine tuliokuwepo katika mazungumzo ya mwisho baada ya kupata ripoti ya kocha Nabi,” alisema bosi huyo.

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alizungumzia hilo la usajili wakati akizungumzia usajili wa Bacca na kusema kuwa; “Kama mchezaji ameonyesha kiwango bora, kama uongozi hatutasita kumuongezea mkataba mpya.

“Lakini kama mchezaji ameshindwa kuonyesha ubora wake kila anapopata nafasi ya kucheza katika timu, basi hatutasita kuachana naye kwa kumpa mkono wa kwa heri, lakini Bacca yeye ameonyesha ubora wake hivyo tutamuongezea mkataba mktaba mpya muda wowote, hivi sasa tupo katika mazungumzo kwa ajili ya kumuongezea mkataba mpya,” alisema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: