Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatenga saa 96 kuisambaratisha Simba

Yanga Tizi Geita Yanga yatenga saa 96 kuisambaratisha Simba

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa siku nne sawa na saa 96 zinamtosha kabisa kuandaa kikosi kitakachoipa matokeo mazuri timu hiyo dhidi ya Simba, katika Kariakoo Dabi.

Dabi hiyo inatarajiwa kuchezwa Jumapili hii saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kwake anauchukulia umuhimu kila mchezo ukiwemo uliopita wa Ligi Kuu Bara waliocheza dhidi ya Kagera Sugar na kuwafunga mabao 5-0.

Nabi alisema jana Jumatano ameanza maandalizi ya mchezo huo, hivyo maandalizi hayo atayafanya kwa siku nne hadi Jumamosi atakapomaliza program zake.

“Nianze kwa kuwapongeza wachezaji wangu kwa kucheza kila mchezo kwa morali ya juu ambayo inanifanya niwe na matumaini ya kupata ushindi katika dabi ijayo.

“Katika mchezo huu tutaingia uwanjani tukiwa tunawaheshimu Simba ni timu yenye mabadiliko lakini hatuwezi kuwa na presha hata kidogo, tutakwenda kuandaa timu itakayokuja uwanjani kucheza kwa ubora mkubwa kwenye mechi hii kubwa, tunawajua vizuri sana.

“Nirudie kusema kuwa, tunaiheshimu Simba na hautakuwa na mchezo rahisi, lakini niseme Yanga itaingia uwanjani kucheza kwa ubora mkubwa kwa ujazo wa mchezo mkubwa kama huo ili tupate ushindi,” alisema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: