Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yatenga bajeti ya Sh20 bilioni msimu ujao

IMG 4431 Makombe Yanga.jpeg Makombe waliyobeba Yanga Msimu 2022/23

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Yanga imetenga bajeti ya Sh 20.8bilioni kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano mbalimbali ya ndani na ya kimataifa.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Fedha, Sabri Sadick amesema ana amini kupitia bajeti hiyo italeta tija kwao msimu ujao na kuweza kufanya vizuri zaidi.

"Katika vyanzo vya mapato tuna Sh 14.8bilioni hivyo tuna upungufu wa Sh 6bilioni ambazo tunaamini tutafanyia kazi kwa haraka iwezekanavyo kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali ili kufikia malengo tuliyojiwekea."

Aidha Sabri aliongeza kiasi hicho ni zaidi ya msimu uliopita kwani timu hiyo ilitumia Sh 17.8bilioni huku matumizi kwa msimu mzima yakiwa ni Sh 17.3bilioni.

"Hadi sasa kiasi cha fedha zilizobaki kwa msimu uliomalizika ni Sh 581milioni, hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa ili kuongeza ufanisi zaidi kwa timu yetu msimu ujao,"amesema.

Katika matumizi ya msimu uliopita Sabri amesema fedha hizo zimetokana na udhamini, kiingilio cha milangoni, ada za wanachama, zawadi ya ushindi, mauzo ya wachezaji, faida ya jezi, mikopo na mapato mengine.

Yanga Inafanya mkutano wake mkuu leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) ikiwa ni wa kwanza tangu uwaingize madarakani Rais wa klabu hiyo, Hersi Said, Makamu wa Rais, Arafat Haji na wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa Julai mwaka jana.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: