Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yashika hatma ya Mbeya City

Msigwa: Kila Kitu Kimekamilika Safari Ya Yanga Algeria Yanga yashika hatma ya Mbeya City

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa Mbeya City, Paul Nonga amesema mchezo wa kesho Jumanne dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ndio utakaotoa taswira kwa timu hiyo kusalia Ligi Kuu.

Nonga amesema endapo watapoteza watakuwa wamekaa kwenye mazingira magumu ya kushuka daraja au kucheza hatua ya mtoano sababu mchezo wa mwisho wanakutana na KMC ambayo haiko nafasi nzuri.

Mbeya City inashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 30 huku KMC ikiwa nafasi ya 13 kwa alama 29 sawa na Mtibwa Sugar ambayo leo itacheza na Kagera Uwanja wa Manungu.

"Tupo tayari kwaajili mchezo ambao ni muhimu sana kwetu kupata ushindi japo tunajua tunakutana na timu bingwa, nzuri na imara lakini kwetu ndio tunauhitaji zaidi.

"Tunauchukulia kwa tahadhari kubwa mchezo huo japo utakuwa na presha na soka ni mchezo hivyo tutajitahidi tusifanye makosa ambayo yatatugharimu," anasema Nonga.

Hata hivyo kipa wa Mbeya City, Ibrahim Isihaka amesema mapumziko ya wiki mbili yamewasaidia kujiimarisha kutokana na safari walizokuwa wakizifanya Kanda ya Ziwa.

Kiingilio katika mchezo huo ni Sh5,000 na milango itafunguliwa kuanzia saa 4 asubuhi.

Katika michezo 15 timu hizo kukutana Mbeya City imeshinda mchezo mmoja kwa mabao 2-1 uliochezwa Uwanja wa Sokoine Novemba 2, 2016 huku City ikifungwa michezo nane na sare sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: