Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yapaa, yawafuata Bamako Mali

DJUMA AUCHO Yanga yapaa, yawafuata Bamako Mali

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumaliza kete yao ya Ligi Kuu Bara Februari 22, 2023 kwa kusepa na pointi tatu mazima msafara wa Yanga umeanza safari kuelekea Mali.

Februari 22 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma KMC 0-1 Yanga na kuipa pointi tatu Yanga ikiwa inaongoza ligi.



Bao pekee la ushindi lilifungwa na Clemnt Mzize akiwa ndani ya 18 akitumia makosa ya kipa wa KMC David Kissu kwenye harakati za kuokoa kona.

Leo Yanga imeanza safari kuelekea Mali kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako unaotarajiwa kuchezwa Februari 26, 2023.



Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye msafara huo ni Tuisila Kisinda, Farid Mussa, Aziz KI, Fiston Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: