Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yamfuata straika rasta

YANGA 01 Yanga yamfuata straika rasta

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mabosi wa timu ya Ihefu FC, wakiendelea kujiridhisha na uwezo wa straika wao mwenye rasta raia wa Burkina Faso, Yacouba Sogne, mabosi wake wa zamani Yanga, wanadaiwa kurejesha nia ya kumsajili kwenye dirisha kubwa lijalo ili akaongeze nguvu kwa Fiston Mayele na Kennedy Musonda.

Tangu ajiunge na Ihefu, Yacouba amefanikiwa kufunga mabao mawili na kutoa asisti moja huku akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Februari.

Yacouba alijiunga na Ihefu kwenye dirisha dogo mwaka huu kama mchezaji huru akitokea Yanga kufuatia kukosa nafasi katika kikosi cha kocha Nasraddine Nabi, mara baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha yaliyomuweka nje karibia mwaka mzima.

Chanzo chetu kutoka Yanga kimesema kwamba, tayari mabosi wa timu hiyo wameonyesha hali ya kuvutiwa na kuimarika kwa Yacouba jambo linalowafanya kumuita mezani upya ili wamrejeshe kikosi msimu ujao huku Ihefu nao wakiweka ngumu kumuachia.

“Kufuatia maelekezo ya kocha Nabi, kuna uwezekano tena wa kumrejesha Yacouba kikosini mwetu msimu ujao, maana tayari anaona mwenendo wake unamvutia na kwamba amesema yawezekana akaja kuongeza nguvu kikosini katika upande wa washambuliaji,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kumtafuta Kocha wa Ihefu, Zubeir Katwila ambapo alisema: “Kwa sasa bado tupo kwenye maboresho ya kikosi chetu, hivyo hatuko tayari kumuacha mchezaji yeyote kama Yacouba ambaye tayari ameshaonekana kufanya vizuri.

“Mpango wetu ni kuhakikisha mchezaji yoyote aliyeonyesha kiwango anabaki ili msimu ujao tuongeze wachezaji wachache katika nafasi maalum,” alisema Katwila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: