Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yakusanya Tsh bil 17.3

Eng. Hersi Yanga Meeting Eng. Hersi Said

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga unaendelea ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam, klabu imetangaza mapato na matumizi kwa msimu uliopita huku wakitangaza bajeti kwa ajili ya msimu wa 2023/24.

Katika msimu uliopita, Yanga ilikusanya jumla ya Tsh Bilioni 17.8 huku matumizi yakiwa Tsh Bilioni 17.3.

Mchanganuo wake ni; Udhamini Bilioni 8.1, Mapato ya mlangoni Bil 2, Ada za uanachama Mil 939, Zawadi Bil 1.1, Mauzo ya wachezaji Mil 200, faida ya jezi Mil 337, Mengine Tsh Milioni 150, mikopo Bil 4.08.

Baadhi ya matumizi ni pamoja na Mishahara Bil 5.4, ada za wachezaji Bil 2.4, motisha 2.8Bil, kambi Milioni 460, Chakula na Malazi Bil 1.1, maandalizi ya mechi Bil 1.4, usafiri Bil 1.6, kodi nyumba Mil 290, Matibabu Mil 102. Jumla matumizi Bil 17.3 na kubakiwa na Mil 581.

Bajeti ya msimu ujao makadirio ya matumizi ni Tsh Bil 20.8 wakati mapati ni Tsh 14.8, uongozi wa Yanga umepewa jukumu kupitia vyanzo vingine kupata fedha kukamilisha bajeti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: