Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yajibu tetesi za kuporwa Fabrice Ngoma na Simba Airport

Fabrice Ngoma Tt Yanga yajibu tetesi za kuporwa Fabrice Ngoma na Simba Airport

Wed, 5 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said ameonyesha kushangazwa na taarifa zinazosambazwa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa klabu hiyo imepokonywa mchezaji na wapinzani wao, Simba Sc.

Hersi amesema hayo leo baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mchezaji Fabrice Ngoma aliyekuwa asajiliwa na Yanga amepokonywa juu kwa juu na kuchukuliwa na Simba akiwa Uwanja wa Ndege Dar.

“Hatuna sababu ya kutolewa mchezo sisi mara nani maana nimesikia taarifa nyingi lakini ndio wakati wenu wana habari kuleta taarifa za tetesi kuhusu usajili.

“Kama mchezaji anaweza kuibiwa airport tujiulize credibility ya huyo mchezaji ipo wapi? Kama umekuja kwa ajili ya dhamira ya kufanya kitu ‘A’ halafu heti unafika airport mtu anakuteka unakwenda kufanya kitu ‘B’, credibility ya huyo mchezaji ikoje?

“Sidhani kama vitu kama hivyo vinaweza kutokea lakini ndio wakati wa tetesi, sisi tunasema ziendelezwe tu lakini tutabaki kwenye uhalisia, mchezaji ambaye tumemsajili atafuata taratibu zetu na kuja kucheza kwenye klabu yetu,” amesema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: