Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaingizwa Super League

Karia Wallace Rais Rais wa TFF, Wallace Karia

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema mwakani 2024 kupitia mashindano ya African Football League (Super League) Yanga itakuwa moja wapo ya timu zitakazoshiriki kwani wanategemea kuwa na timu 24.

"Kwa mwaka huu tuna timu nane lakini makubaliano ni timu 24, ukanda wa CECAFA na COSAFA tunatakiwa kutoa timu nane mwakani hata Yanga itakuwepo,"

Karia pia amewapongeza maofisa habari wa timu zinazoshiriki michuano ya CAF ngazi ya klabu Ally Kamwe (Yanga), Ahmed Ally (Simba) na Hussein Massanza (Singida Fountain Gate) kwa kuungana kwa pamoja katika kufanya hamasa kuelekea katika michezo yao.

Aidha amezitaka klabu hizo kwenda kuwakilisha nchi vyema kwani katika mashindano ya kimataifa nchi ndio inashiriki.

"Naamini timu zetu zitafanikiwa kuingia makundi katika mashindano ya kimataifa na hayo ndio malengo yetu, Timu zinapocheza mashindano ya kimataifa tunaenda kama Tanzania tukirudi kwenye ligi yetu kila mtu apambane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: