Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaifuata Singida B.S kibabe

Yanga Vs Rivers United Yanga yaifuata Singida B.S kibabe

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha wachezaji wa Yanga na benchi la ufundi kimeondoka jioni ya leo kuelekea Singida ambapo wamesafiri kwa ndege mpaka Dodoma na baada ya hapo wataunganisha na basi mpaka Singida.

Yanga itakuwa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa Mei 4, kwenye dimba la Liti ambapo Yanga itakuwa ikisaka alama 3 muhimu kuelekea kutwaa Ubingwa wa 29 wa Ligi.

Mpaka sasa Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa imeshacheza michezo 26, na kushinda michezo 22, kutoa sare michezo 2 na kupoteza 2 huku wakiwa wamejikusanyia alama 68.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: