Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yahamia robo fainali CAFCC

Wachezaji Yanga 1 1140x640 Yanga yahamia robo fainali CAFCC

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa klabu ya .Hersi Said amesema kuwa wamejipanga kuwekeza nguvu kwenye maandalizi ya timu yao ili kufanya vizuri kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa anajua wanapoelekea ni pagumu zaidi ya walipotoka ndio maana wameamua kuwekeza mapema kwenye maandalizi ili kulipa nafasi benchi la ufundi kujenga timu ya ushindani.

“Malengo ya Yanga yalikuwa ni kufika robo fainali lakini kwa mwenendo wetu kwenye mechi za hatua ya makundi imetupa hamasa na kuona kama tunaweza kufika mbali zaidi ndio maana tumekusudia kuongeza ukaribu na benchi la ufundi ili kutekeleza mahitaji yao na kutuandalia timu ya ushindani itakayotupa tunachokitaka huko tunapoelekea,” amesema Rais wa Yanga, Eng.Hersi Said.

Kikosi cha Yanga kimeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe pamoja na mechi za Ligi Kuu na Kombe la FA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: