Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yafunguka kitendo cha Morrison kwenda Kambini Avic Town

Morrison Skudu28242 Yanga yafunguka kitendo cha Morrison kwenda Kambini Avic Town

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imefafanua kitendo cha aliyekuwa mchezaji wake, Bernard Morrsion raia wa Ghana kwenda katika kambi ya timu hiyo, Avic Town Kigamboni Dar na kusalimiana na wachezaji licha ya kuwa ameshapewa mkono wa kwa heri na klabu hiyo.

Akifafanua hilo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wachezaji karibia wote waliocheza Yanga wanajisikia wapo nyumbani hata kama wamemaliza utumishi wao ndani ya klabu hiyo hivyo wanakaribishwa na wajisikie kama wapo nyumbani.

"Ni tamaduni ambayo tunayo Yanga, hatusemi kwa wachezaji wote lakini kwa asilimia kubwa wachezaji wanaocheza Yanga hapa huwa nyumbani kwao. Hata ikifika wakati kwamba mchezaji amemaliza muda wake, Yanga huwa ni nyumbani kwake.

"Hii inatokanaa na mambo mengi ikiwemo upendo anaoupata kutoka kwa mashabiki, mazingira anayopata kutoka kwa viongozi, maisha ya kambini na alivyozoeana na wachezaji wenzake.

"Kwa hiyo licha ya kumalizana na Yanga, Bernard Morrison alihitaji kwenda kambini. Morrison alipewa 'thank you' yake msimu ukiwa umemalizika. Hivyo alihitaji kwenda kambini kusalimiana na wachezaji wenzake na kuagana nao vizuri.

"Lakini aliposikia kwamba Yanga imemsajili mwalimu wa walimu kwenye shibobo, Skudu Makudubela ambaye ndiye mwalimu wake aliyemfundisha mpaka ile kupanda mpira mlivyokuwa mkimuona.

"Morrison akaona acha nikamtembelee mwalimu wangu Skudu, wamesalimiana vizuri na Skudu akampa jezi Morrison naye amefurahi, tunamtakia kila la heri kwenye maisha yake mapya ya soka ambako anakwenda, lakini mwenyewe anajua Yanga ni nyumbani na muda wowote anakaribishwa akiwa anahitaji," amesema Kamwe.

Morrison aliwahi kucheza na Skudu katika Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini kabla ya Morrison kutimkia AS Vita kisha Yanga na baadaye SImba kabla ya kurejea tena Yanga msimu uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: