Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaanza jeuri: Wa kutuzia nani?

Yanga Y00 Kikosi cha Yanga

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ushindi wa bao 1-0 walioupata Yanga juzi jijini hapa mbele ya wenyeji wao, TP Mazembe umewaibua mashabiki wa timu hiyo na kutoa kauli ya kibabe kuwa hakuna timu ambayo inaweza kuwazuia isiwape kichapo kokote pale itakapokuwa iwe ugenini au nyumbani.

Kauli hiyo ilikuja muda mfupi baada ya timu hiyo kupata ushindi huo ukiwa ni mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao ulipigwa katika Uwanja wa Mazembe, jijini hapa.

Bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo ambao iliwakosa baadhi ya wa nyota wake wa kikosi cha kwanza lilifungwa na kiungo Farid Mussa akitumia makosa ya kipa wa Mazembe baada ya kuicheza vibaya krosi ya winga Jesus Moloko.

Kabla ya kupata bao hilo Yanga walikuwa wanaliandama lango la Mazembe kupitai kwa nyota wao watatu, Fiston Mayele, Kennedy Musoda na Muadhathir Yahya ambao walitengeneza majaribio kadhaa lakini umakini wa mlinda mlango wa TP Mazembe ulizima hatari hizo.

Baada ya kupata ushindi huo Yanga ilifikisha pointi 13, ambapo walikuwa wanasubiri mechi ya wapinzani wao US Monastir ambao walikuwa wakicheza dhidi ya Real Bamako kwa ajili ya kufahamu timu gani ambayo ingemaliza kileleni mwa msimamo wa kundi D la michuano hiyo kati yao au Monastir.

Katika mchezo huo, Yanga iliwakosa mastaa wake, Stephane Aziz Ki, Djigui Diarra, Khalid Aucho sambamba na kocha wao mkuu, Nasreddine Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: