Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ya Gamondi ni zaidi ya Yanga na Nabi

Nabi Gamondi 2 WA0002 Yanga ya Gamondi ni zaidi ya Yanga na Nabi

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpaka sasa nimetazama michezo (2) ya Yanga ya Gamondi kwa dakika (180') dhidi ya Kaizer Chiefs na Azam FC, nimebaini haya;

◉ Yanga ya Nabi na Gamondi zinafanana kwenye falsafa, wanacheza soka la burudani 'possession football'.

◉ Yanga ya Gamondi ina tofauti moja dhidi ya Yanga ya Nabi, kasi pace, intensity.

Yanga ya Gamond inamiliki huku inatembea kwa kasi na intensity kubwa kwenda mbele hasa baada ya ujio wa Yao & Maxi Nzengeli ambao wana energy kubwa, wanatembea eneo kubwa uwanjani kwa kasi ileile mwanzo hadi mwisho, tunaita wana mapafu ya farasi.

Yanga ya Nabi ilikuwa slow kidogo, inaanzia chini taratibu huku kasi ikiongezeka hasa wanapofika kwenye nusu ya mpinzani.

◉ Kama Nabi, hata Gamondi leo amefanya mabadiliko ambayo yamemlipa. Alimuinua Aziz Ki, akafunga goli. Akamuinua Walid Mzize ambaye nae alifunga goli pia.

Katika dakika za mwisho nimeona kitu kipya kingine kwa Gamondi, high pressing very very organized, high intensity.

Ana wiki kadhaa na timu, baada ya miezi (2) tutam-judge zaidi, lakini kwa sasa nimeona hayo kwenye Yanga ya Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: