Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ya Gamondi inakaba mpaka kivuli

Yao Gamondi Yanga ya Gamondi inakaba mpaka kivuli

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Timu ya Yanga, jana ilifungua pazia la Ligi Kuu kwa ushindi mzito wa bao 5-0 dhidi ya KMC.

Wengi hawajastaajabu Yanga kupata ushindi huo bali namna walivyoweza "kuicontrol" mechi kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho katika mchezo huo.

Kitu ambacho Yanga iliwapa shida wageni wao KMC ni mfumo wao wa kukaba kwa nguvu na kunyang’anya kwa haraka mpira kutoka kwa wapinzani wakihakikisha wapinzani wao hawasogei kwenye eneo lao la hatari.

Hatua hiyo iliwapelekea KMC muda mrefu kushindwa kutoka katika nusu uwanja yao na walipojaribu kuvuka kwenda nusu ya Yanga walipoteza mpira kwa haraka. KMC ilionekana kupata shida katika dakika 30 za kwanza ambapo hawakufanikiwa kufika eneo la hatari la Yanga kwa shambulizi lolote.

Wageni hao walifika kwa mara ya kwanza eneo la hatari dakika ya 31 kwa krosi ya beki wao wa kushoto Rahim Shomari akimtafuta mshambuliaji wake Sadala Lipangile lakini hata hivyo beki Dickson Job aliidhibiti kirahisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: