Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watua salama Dubai, waanza Safari kuelekea Tunisia

Yanga Dubai Msafara wa Kikosi cha Yanga wakiwa Dubai

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Wananchi Yanga imefika salama Dubai baada ya kuanza safari ya kutoka hapa nchini Tanzania majira ya jioni ambapo itapumzika hapo (Dubai) kabla ya kuanza safari ya kuelekea Tunisia.

Yanga inaenda Tunisia kwa ajili ya kucheza mechi ya kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Monastir siku ya Jumapili majira ya saa moja kamili usiku katika dimba la Olympique Hammadi Agrebi mjini Radès.

Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo wa pili Februari 19 dhidi ya TP Mazembe ya Congo kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi hilo mzunguko wa kwanza kwa kukipiga na wenyeji, Real Bamako nchini Mali Februari 26.

Mzunguko wa pili Yanga itaanza nyumbani dhidi ya Real Bamako Machi 8, kabla ya kuwapokea Monastir Machi 19 na kwenda kukamilisha mechi za kundi hilo Jijini Lubumbashi mbele ya TP Mazembe Aprili 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: