Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga washtukia hujuma ya TP Mazembe

YANGA DUBAI 1 1140x640 Yanga washtukia hujuma ya TP Mazembe

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Klabu ya Yanga ikiwa safarini kwa ajili ya kukamilisha ratiba ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya TP Mazembe, uongozi huo kupitia kwa Ofisa Habari wake, Ally Kamwe, umesema kuwa umeamua kusafiri na msafara wa watu 40 ili kukabiliana na hujuma zozote zitakazojitokeza.

Yanga ipo nafasi ya pili katika kundi (D) ikiwa na pointi 7, huku US Monastir ya Tunisia ikiongoza kundi kwa pointi 10 wakati TP Mazembe ikiwa na pointi 3 na Real Bamako wakuburuza mkia wakiwa na pointi 2, jambo ambalo linawafanya Yanga, kuwa na nafasi ya kutofungwa na TP Mzembe baada ya mchezo wa kwanza katika Uwanja wa Mkapa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Akizungumza nasi, Kamwe alisema, tayari wameshajipanga kikamilifu kukabiriana na hujuma zote katika mchezo huo, ndiyo maana wameamua kuondoka na msafara wa watu 40, nje ya wachezaji waliopo DR Congo na Musonda ambaye alikuwa timu ya Taifa ya Zambia ambao wataungana na timu huko huko.

“Tunamshukuru Mungu msafara wetu upo safi na kwamba hadi sasa hakuna majeruhi hata mmoja ndani ya klabu ambaye hajarejea, hivyo tunaenda DR Congo kutafuta ushindi ili tuweze kukamilisha makundi katika nafasi nzuri, tayari Mayele yuko huko tutaungana naye akiwa sambamba na Kennedy Musonda pamoja na Aziz Ki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: