Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wanapambana usiku na mchana kumbakisha Mayele

Fiston Kalala Mayele Life Mayele

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dau analotaka mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Mayele limewafanya mabosi wa Yanga kukuna kichwa kwani ni wazi kuwa ofa yake imekuwa kubwa kutokana na kiwango bora alichokionyesha katika misimu miwili mfululizo

Kwa sasa ni timu nyingi zimetajwa kumtaka mshambuliaji huyo mwenye tuzo ya ufungaji bora wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Imeelezwa kuwa timu moja kutoka Afrika Kusini imetuma ofa nono ikimtaka mshambuliaji huyo huku timu kadhaa za kutoka Mataifa ya kiarabu zikimtaka pia.

Pamoja na ofa nono ambazo zinamiminika Jangwani mabosi wa Yanga wanafanya juu chini kumbakisha mshambuliaji huyo.

Mayele aliporejea kutoka katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya DR Congo aliitwa na mabosi wa Yanga na kukaa mezani kujadili kuhusiana na ofa zilizopo mezani lakini pia Yanga wakiwa wameweka ofa yao kwa mchezaji huyo aliyebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa Yanga wametoa dau la mshahara wa dola za Marekani 12,000 (Tsh milioni 28) lakini Mayele amekataa akitaka kulipwa dola 15,000 (Tsh milioni 35) kwa mwezi.

Kama makubaliano yatafikiwa huenda siku ya Jumamosi kwenye mkutano mkuu, wanachama wakakutana na habari njema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: