Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamefanya jambo la busara kumuuza Mayele - Job

Fiston Kalala Mayele Tt Fiston Mayele.

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, George Job ameupongeza uongozi wa Klabu ya Yanga kwa namna ambavyo umemaliza kwa weredi wa hali ya juu suala ya mshambuliaji wao Fiston Mayele.

Mayele ambaye ni raia wa Congo anatajwa kumalizana na uongozi wa Yanga baada kuuzwa katika klabu ya Pyramids FC ya nchini Misri kwa kitita cha dola za za Kimarekani milioni 1.2.

Job amesema biashara ya Mayele kwenda Pyramids imevunja rekodi kwani hakuna mchezaji nchini Tanzania ambaye amewahi kuuzwa kwa pesa ndefu kiasi hicho.

"Niupongeze uongozi wa Yanga kwa kufanikisha dili hili kubwa la rekodi ya nchi, USD $ milioni 1.2 (Tsh bilioni 2.8) kwa mchezaji aliyebakisha mwaka mmoja tu kwenye mkataba ni zaidi ya faida.

"Hata Pyramids wangetoa USD $ 500K, Yanga wangekuwa wanepata faida kwa sababu Mkataba wa Mayele ulikuwa umebakia mwaka mmoja. Kutoka $ 500K hadi $ milioni 1.2 Yanga wamefanya jambo kubwa sana, nawapongeza viongozi.

"Nimependa sana jinsi mchezaji mwenyewe (Mayele) na uongozi walivyoliendea jambo hili, very professional. Hujasikia maneno maneno yoyote tofauti na wachezaji wetu.

"Wakati wote hata sasa ukimuuliza Mayele hatma yake anakujibu 'Klabu yangu ndio itaamua' hasemi ataondoka au atabaki," amesema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: