Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga walikuwa bora, Simba walinyimwa penati

Aucho Kibu Yanga walikuwa bora, Simba walinyimwa penati - Edo Kumwembe

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe amesema kuwa kikosi cha Yanga SC walikuwa bora kwenye mchezo wa jana wa Fainali ya Ngao ya Jamii kuliko wapinzani wao Simba SC licha ya kutolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Kumwembe amesema kuwa, intersection iliofanywa kiungo wa Yanga, Khalid Aucho kwa Kibu Denis katika ndani ya box la Yanga, likikuwa ni penati moja kwa moja kwa kuwa haikua mchezo wa kiungwana.

Mchezo huo ulimalizika dakika 90 kwa timu zote kutoka sare ya bila kufungana hivyo wakalazimika kwenda kwenye changamoto ya mikwaju ya penati ambapo Simba walifanikiwa kushinda kwa kufunga penati 3-1.

"Nimegundua machache leo, watani wote wawili hawawezi kupiga penalti, Yanga walikuwa bora kuliko Simba, Simba walinyimwa penalti katika dakika 90, yule Yao, beki wa kulia wa Yanga bonge la beki. Note: Hatuhitaji kujadili bao la Yanga. clear offside," amesema Edo Kumwembe.

TAKWIMU ZA MCHEZO

Yanga -------------- Simba

01 ....... On target ....... 01

05 ....... Off target ...... 01

07 ......... Corner ........ 01

13 ......... Fouls ......... 13

06 ........ Off-side ....... 00

00 ..... Yellow cards ...... 02

56 ....... Possession ...... 44

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: