Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waendelea pale pale walipoishia, waichapa JKT TZ bao 5

IMG 5509 Yanga Bao 5 Nzengeli.jpeg Maxi Mpia Nzengeli amefunga mabao Mawili katika ushindi wa mabao 5-0

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu ya Yanga wameendelea kugawa dozi ya bao 5 michezo yake ya Ligi Kuu Bara 2023/24.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, umewashuhudia wababe hao wakiibuka na ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania.

Mabao ya Yanga katika mchezo wa leo yamefungwa na Stephen Aziz KI, Kennedy Musonda, Yao Attohoula na Maxi Nzengeli aliefunga mabao mawili.

Huu ni mchezo wa pili wa Likgi kwa Yanga msimu huu baada ya ule wa kwanza ambako waliichapa KMC mabao 5-0.

Kwa ushindi huo Yanga wanafikisha alama 6, na kujikita katika kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwazidi Simba na Azam kwa idadi ya mabao ya kufunga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: